SIMORIX THE GENERAL, WEUSI WAACHIA REMIX YA VACCINE | ZamotoHabari

MSANII nyota wa Muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Australia, Saimoni Masanja, Simorix The General, amekuja kivingine na wimbo Vaccine Remix aliowashirikisha wasanii wa kundi wa Weusi la nchini Tanzania.

Akizungumza  Simorix The General, amesema huo ni mwendelezo wa mpango wake wa kuliteka soko la Bonito pia kuipisha lugha ya Kiswahili nchini Australia kupitia muziki.

“Muda wowote kutoka sasa video ya Vaccine Remix itakuwa hewani, nimefurahi kuona audio imepokewa vizuri na mashabiki kutoka kwenye mitandao yote ya kusikiliza na kupakua muziki, naamini hii ni hatua kubwa kwenye muziki wangu kufanya kazi na kundi bora la Hiphop Weusi,” amesema Simorix.

Aidha amesema kuwa katika kuonyesha mwendelezo wa kuitangaza Lugha ya kiswahili nchini Australia, Samorix ameibiluka kivingine na wimbo Vaccine Remix aliowashirikisha G Nako, Nikki wa Pili, Joh Makini na Lord Eyers.

Wimbo huo Mara ya kwanza ulitoka mwaka huu February 14 mwaka huu katika msimu wa Valentine day na baada ya muda mrefu kupita aliwashirikisha kundi la Weusi.

"Ninauwezo wa kufanyakazi na msanii au kundi lolote lile lakini mashabiki walipendekeza  nifanye kazi na kundi la weusi kwa kuwa hill kundi hata na Mimi nalipenda hivyo ikawa rahisi kufanya nao kazi."amesema Simorix

 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini