Na Farida Mangube, Morogoro .
Waziri wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo kutoka serikali ya mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita, anatarajiwa uwa mgeni rasmi Mashindano ya 16 Michezo ya Bandari (Interport games) yanatarajiwa kutimua vumbi septemba 26 mwaka huu mkoani Morogoro katika viwanja vya Jamhuri na viwanja vya chuo cha waislamu vya mjini Morogoro.
Mashindano hayo yatashirikisha Taasisi nne za bandari zikiwa na timu tano ambazo zitacheza mpira wa miguu, mchezo wa kamba, riadha, pamoja na mpira wa kikapu.
Akizungumza na waandishi wa habari juu mashindano hayo Meneja rasilimali watu TPA na Mwenyekiti wa kamati ya Michezo ya Bandari Mussa Msabimana alisema mashindano hayo ambayo yanafanyika kila Mwaka na kwamba lengo ni kuwaweka pamoja wafanyakazi wa TPA kutoka bandari zote nchini kupitia michezo, ambapo watapata wasaa wa kubadilishana uzoefu .
Kwa upande wake mratibu wa michezo ya bandari Keny Mwaisabula na mkufunzi wa mchezo wa pete michezo ya bandari Judith Irunda walisema maandalizi yamekamilika Kwa timu zote ambazo kwa sasa zinasubiria mashindano hayo kuanza na kila timu imejipanga kushindana na sio kushiriki.
Katika mashindano hayo Michezo kadhaa imeongezwa ili kuongeza ushindani wa mashindano ya bandari ikiwa ni pamoja na ongezeko la bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kutarajiwa kutumika katika mashindano kwa ujumla
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments