SILENT OCEAN WAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA THAMANI YA MILIONI 13.4/- KWA JESHI LA POLISI | ZamotoHabari


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KAMPUNI ya Silent Ocean Kilimanjaro Star Cargo imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.Milioni 13.4 kwa majeshi ya Polisi ya Tanzania yanayoshirikiana na majeshi ya nchi mbalimbali za ukanda wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo kwa sasa wanaendelea na michezo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo zikiwemo jezi jozi 150 pamoja na mipira mitano mitano kwa kila timu za majeshi hayo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo Mohamed Kamilagwa amesema wamekabidhi vifaa hivyo kama sehemu ya kuunganisha nguvu za kuliwezesha Jeshi la Polisi kushiriki kikamilifu kwenye michezo inayohusisha majeshi ya polisi zilizopo nchi za SADC.

"Katika ushirikiano wetu na Jeshi la Polisi tumechangia vifaa vya michezo vyenya thamani ya Sh.miloni 13.4 kwa ajili ya kusaidia vifaa hivyo hususani jezi na mipira, tunaamini ni mchango mdogo lakini utakuwa chachu kwa wadau wengine kulisaidia jeshi katika michezo mbalimbali.

"Kwa hiyo tunafuraha kuwa sehemu ya Mashindano haya na tunatarajia yataleta morali ya ushindi katika timu zetu za Jeshi la Polisi Tanzania na kuweza kugeuka vinara katika mashindano haya yanayoshiriki majeshi ya polisi kwa nchi za Ukanda wa SADC.Mashindano haya moja ya engo lake ni kujenga udugu na shikamano na kuyaimarisha majeshi yetu,"amesema.

Ameongeza Kwa hiyo wao kama wadau wa biashara wameona kwamba kwao ni fursa kuungana na Jeshi letu na kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP pamoja na Rais kwa ajili ya kuwafanya walioko kwenye majeshi hayo wajenge familia iliyoshikamana Ukanda wa SADC.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo vya michezo , Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Interpol Kitaifa Jemini Mushy amesema vifaa walivyopokea vitasaidia kufanikisha michezo iliyoandaliwa na Shirikisho la Polisi ukanda wa Kusini wa Afrika.

"Ni michezo ambayo inalenga kujenga uhusiano zaidi na wanaoshiriki wengi katika hii michezo ni askari vijana ambao watakuwa majeshini kwa muda mrefu, vikao vingi vinafanyika ambavyo vinashirikisha wakuu ambao mara nyingi ni wachache ,kwa hiyo wanapata nafasi ya kukutana wao kwa wao.

"Kwa hiyo michezo imewakutanisha askari wa chini ambao ndio wanapambana na uhalifu unaovuka mipaka, kwa Kampuji ya Silent Ocean tunawashukuru sana kwani ni miongoni mwa wadau ambao wamejitoa kimasomaso kuhakikisha tunakuwa na vifaa vinavyohitajika kwenye hii michezo hii,"amesema

Ameongeza hiyo inaonesha nia halisi ya kampuni hiyo katika kupambana na uhalifu lakini pia kuunga mkono Polisi kwa mambo mazuri tunayofanya na kwamba vifaa hivyo vitawasaidia askari kufanya vizuri kwenye michezo na hata baada ya Mashindano hayo vingine vitaendelea kutumika kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa vijana wao(askari) wawe atika hali nzuri ya michezo

"Niwaombe wadau wengine waendelee kujitolea kwa namna hii kwa ajili ya kuliwezesha Jeshi lao kwasababu unapozungumzia Polisi jamii pamoja na kufanya doria na kupambana na uhalifu moja kwa moja lakini njia hii ni moja ya kupambana na uhalifu kwani askari watakapokuwa wanashiriki kwenye michezo wanatoa funzo kwa jamii lakini ni katika kuimarisha ushirikiano wa Ukanda wa Kusini."

Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Interpol  Kitaifa Jemini Mushy( wa pili kushoto) akiwa  na maofisa wa wengine wa Jeshi hilo pamoja na  Mwakilishi wa Kampuni ya Silent Ocean Mohamed Kamilagwa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo katika Kampuni hiyo( katika)wakiwa wameshika vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni hiyo.

Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Interpol  Kitaifa Jemini Mushy akizungumza kabla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya majeshi ya Jeshi la Polisi yanayoshiriki michezo mbalimbali katika nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC).Wa pili kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya Silent Ocean Mohamed Kamilagwa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo katika Kampuni hiyo.

Mwakilishi wa Kampuni ya Silent Ocean Mohamed Kamilagwa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo katika Kampuni hiyo akitoa maelezo kwa Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Interpol  Kitaifa Jemini Mushy kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya majeshi ya Jeshi la Polisi yanayoshiriki michezo mbalimbali katika nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SADC).

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini