YANGA WASAINI MKATABA MNONO WA BILIONI 10.9 NA KAMPUNI YA GSM GROUP | ZamotoHabari


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga Africans imeingia mikataba miwili na Kampuni ya GSM Group yenye jumla ya thamani ya Sh.bilioni 10.9 katika kipindi cha miaka mitano

Mkataba huo kati ya Klabu Yanga na Kampuni ya GSM Group umeingiwa leo Septemba 12 jijini Dar es Salaam na kwamba makubaliano yaliyoingiwa ni mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Sh.bilioni 9.1 ambao unahisisha utengenezwaji wa jezi mbalimbali na bidhaa nyingine zitakazokuwa na nembo ya Yanga.

Kwa mujibu wa mkataba huo Yanga itakuwa inavuna Sh.bilioni 1.5B kwa kila mwaka kutoka Kampuni ya GSM Group kutokana na mauzo ya kwenye jezi huku ikielezwa pia Yanga itakuwa inavuna asilimia 10 fedha katika kila mauzo ya jezi kwenye kila mwezi.

Wakati huo huo Klabu ya Yanga imeingia mkataba mwingine na Kampuni ya GSM Group kupitia bidhaa zake za GSM Foam. Kutokana na mkataba huo Yanga itakuwa inavuna Sh.milioni 300 kwa kila mwaka katika kipindi cha miaka mitano.Yanga itakuwa inapata mgawo wa asilimia 8.5 ya uongezeko la mauzo kupitia Gsm foam .Pia itapata nyongeza ya fedha kwa kila mwaka Kutoka GSM Foam.

Kutokana na kuingiwa kwa mikataba hiyo , GSM Group itaiwezesha Klabu ya Yanga kupata Sh.bilioni 10.9 katika kipindi cha miaka nitano.
Kwa mujibu wa viongozi wa Yanga na GSM Group ni kwamba Yanga inakuwa timu pekee katika Bara la Afrika kwa Sasa Kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kupata udhamini mnono wa mauzo ya jezi na udhamini mdogo kwenye jezi yao.

Akizungumza kuhusu mikataba hiyo, Rais wa Klabu ya Yanga Eng Hers Said amesema mikata hiyo inakwenda kuinufaisha klabu hiyo huku akieleza kila mwaka fedha zitakuwa zikiongezeka kwa asilimia 10 kutokana na Mauzo ya jezi.

Eng Hers Said amesema kwamba mikataba hiyo sasa itakwenda kuweka usawa ndani ya Klabu ya Yanga kwa kuiboresha mikataba waliyoingia kwa kila mwaka na kuongeza kuwa aliahidi kuipa thamani halisi ya Klabu ya Yanga na mkataba huo ni kielelezo tosha.

Wakati upande wa Kampuzi za GSM Group ambazo zipo chini ya Ghalib said Mohammed umetumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wadau wote ambao wamewapa thamani kubwa kwa sasa sokoni kufanya vizuri.

Aidha GSM Group wametoa shukrani Klabu ya Yanga kwa kuwapatia heshima hiyo kwa sasa na kwamba ni ukweli usiopingika Klabu ya Yanga imewaheshimisha GSM Group na ndio maana wameamua kulipa fadhila kwa kuwaonesha upendo mkubwa kwa kusaini nao tena mikataba ya miaka miwili yenye jumla ya thamani ya fedha Sh.bilioni 10.9.


 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini