WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Mnauye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Kusifu na Kuabudu la Rejoice litakalofanyika Septemba 16,2022 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza na waandishi habari leo Septemba 13, Mlezi wa kwaya ya Moravian Efatha, Yona sonelo amesema maandalizi yamefikia Asilimia 95 Katika kuelekea siku ya tamasha hilo huku wanakwaya mbalimbali wameshathibitisha kuhudhuria tamasha hilo.
"Siku ya Tamasha tarehe 16 ya mwezi wa tisa Mgeni Rasmi atakuwa ni waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye"
Amesema Wanakwaya wa kwaya moravian efatha choir, watawakutanisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka Afrika uwanjani hapo.
Amesema siku ya kesho kwaya Moravian itaanza mazoezi ya mitambo ya sauti na siku ya alhamisi kwaya ambazo zimealikwa watafanya mazoezi ikiwemo kwaya ya joyous celebration kutoka Afrika kusini.
Ameongezea kuwa tamasha la rejoice litaanza kuanzia saa 11 jioni na waimbaji wataanza kuimba mpaka alfajiri ya Tarehe 17 siku ya jumamosi.
Kwa upande wa Usalama siku ya tamasha jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha watu wanakuwa salama muda wote wa tamasha hilo.
Aidha amesema tiketi Bado zinapatikana Katika app ya 'NILIPE' ambazo zinaanzi VIP shilingi milioni moja, laki tano, laki moja, Elfu hamsini na elfu ishirini kwa kawaida.
"Tunawakaribisha watanzania wote Katika Tamasha la kuombea Nchi yetu ya Tanzania na Kwa wengine wanaotaka kununua tiketi uwanjani pia zitapatikana" Amasema Yona sonelo.
Mlezi wa Efatha Moravian kwaya ambaye ndiye muandaaji wa Tamasha la muziki wa Injili Yona Sonero Amesema ulinzi kwenye Tamasha hilo la Rejoice utakuwa ni wa uhakika na amewataka wananchi wafike bila kukosa,
Amesema kuwa wao kama waandaaji wameshafanya mazungumzo na vyombo mbalimbali vya Ulinzi ili kulifanukisha Hilo kwa asilimia mia moja,
Aidha amesema kuwa Kwaya zote maarufu Tanzania zitakuwepo.
Mlezi wa kwaya ya Moravian Efatha, Yona sonelo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati akitambulisha waim baji mbalimbali kutoka hapa nchini na Afrika kunisini pamoja kuelezea maandalizi ya Tamasha la Rejoyce kuwa limekamilika kwa asilimia 95.
Mwimbaji Bupe mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati walipofika katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam kuangalia namna maandalizi ya tamsha la Rejoyce litakalofanyika Septemba 16, 2022. Amesema kuwa wamejianda vyema kutumbuiza katika tamasha hilo siku itakapofika.
Mwalimu wa Kwaya Fredy Masanja Mwimbaji Bupe mwakyusa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati walipofika katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam kuangalia namna maandalizi ya tamsha la Rejoyce litakalofanyika Septemba 16, 2022. Amesema kuwa Ameinoa vyema kwaya yake kwaajili ya kutumbuiza siku ya Tamasha hilo.
Muonekano wa Jukwaa tayari kwa tamasha la Rejoyce Septemba 16, 2022.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments