Kikosi cha KMC FC leo kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa siku ya Jumamosi Oktoba 15 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni inayonolewa na Kocha Mkuu Thierry Hitimana imeingia kambini jana jioni baada ya mapumziko ya siku mbili tangu ilipocheza mechi ya mzunguko wa sita dhidi ya Ruvu Shooting nakutoka sare ya kutokufungana.
KMC inajiandaa katika mchezo huo ikihitaji ushindi baada ya kutoa sare katika michezo miwili ambayo ni dhidi ya Namungo iliyocheza katika uwanja wa Majaliwa Ruangwa mkoani Lindi sambamba na dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salam.
Katika mchezo huo , KMC FC inafanya mazoezi yanayolenga benchi la ufundi kusahihisha makosa mbalimbali yaliyojitokeza katika maeneo ambayo yalionekana kwenye mchezo huo uliopita na hivyo kupelekea Timu kukosa alama tatu muhimu.
"Tunajiandaa na mchezo ambao kimsingi utakuwa mgumu kutokana na kila Timu kuhitaji matokeo, tunawafahamu Mtibwa ni Timu nzuri na hata ukiangalia kwenye mchezo wao uliopita ambao wametoka sare walicheza vizuri na hivyo kama Timu tunajiandaa Ili kupata matokeo mazuri.
" Ukiangalia kwenye mchezo ambao tulitoka sare na Ruvu Shooting wachezaji walicheza vizuri lakini bahati mbaya hatukupata matokeo mazuri lakini tunaamini ubora wa wachezaji wetu, umakini walionao utaleta matokeo chanya kwenye mchezo unaokuja kwasababu KMC tuna kikosi kizuri.
Hata hivyo hadi sasa KMC FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ipo kwenye nafasi ya tisa ikiwa na jumla ya alama saba huku ikiwa imeshacheza jumla ya michezo sita na kwamba kati ya hiyo imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare michezo minne huko ikipoteza mmoja.
Imetolewa leo Oktoba 10
Na Christina mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano KMC.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments