LUGALO GOFU KLABU WAALIKWA MALAWI. | ZamotoHabari

KLABU ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo imeendelea kufanya mazeozi Baada ya kupata Mwaliko kushiriki Mashindano nchini Malawi.

Akizungumza mmoja wa wachezaji wanaotarajiwa kushiriki Shindano hilo Mkuu wa Chuo Cha Ulinzi cha Taifa NDC Meja Jenerali Ibrahim Muhona amesema wapo vizuri na kinachosubiriwa ni Kukamilika Kwa Taratibu zitakazowawezesha kushiriki.

"Kimsingi tunaendelea na mazoezi tunajiandaa na Shindano nchini Malawi na wachezaji wamejitokeza kwa wingi wachezaji wa Malawi walikuja kwetu safari hii tunaenda nchini kuwaonyesha uwezo wetu kwa mara nyingine. "

Hata hivyo amewapongeza klabu ya Lugalo gofu kwa kujiandaa vizuri kushiriki Shindano hilo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema Jeshi linaonyesha Njia na ameziomba taasisi nyengine kushirikiana katika michezo na taasisi za nchini jirani ili kukuza ujirani mwema.

"Leo tumeanza mazoezi na tumefanikiwa kucheza viwanja 18 hivyo tumejipanga vyema kurudi na ushindi na matumani yetu ni kushinda na kufanya ziara ya kudumisha uhusiano mzuri na kuonyesha nchi ya Tanzania wako vizuri katika mchezo wa gofu."

Timu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo inatarajiwa kwenda nchini Malawi baada ya kupata Mwaliko kushiriki Shindano la mchezo wa Gofu litakalo fanyika Mwanzoni mwa Novemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Lugalo  Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo akipiga mpira Wakati akifanya mazoezi Leo Octoba 21,2022 Katika Klabu Hiyo.
Meneja Wa Klabu Ya Jeshi la Ulinzi la wananchi Wa Tanzania-JWTZ Kanali David Mziray Akipiga mpira Wakati akifanya mazoezi Leo Octoba 21,2022 katika klabu hiyo.
Mkuu wa Chuo Cha Ulinzi cha Taifa NDC Meja Jenerali Ibrahim Muhona Akipiga mpira Wakati akifanya mazoezi Leo Octoba 21,2022 Kwenye klabu Ya Jeshi la Ulinzi la wananchi Wa Tanzania-JWTZ Lugalo Golf
 Meneja Wa Klabu Ya Jeshi la Ulinzi la wananchi Wa Tanzania-JWTZ Kanali David Mziray Akipiga mpira Wakati akifanya mazoezi Leo Octoba 21,2022 katika klabu hiyo.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini