MAMIA WAJITOKEZA KUCHUKUA NAMBA ZA KILI i MARATHON DAR | ZamotoHabari


Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani wamejitokeza katika zoezi la utoaji namba za kukimbilia kwa ajili ya Kilimanjaro International Premium Lager  Marathon inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Waandaaji wa mbio hizo wamesema zoezi hilo la siku mbili litahitimishwa kesho Jumapili saa kumi na mbili jioni kwa mkoa wa Dar es Salaam.

“Tumeanza vizuri na ni matumaini yetu kuwa washiriki watazingatia muda uliowekwa ili tuweze kuwahudumia kwa siku mbili hizi kabla hatujahamia Arusha,” amesema Rajon Datoo, msimamizi wa zoezi hilo kutoka kampuni ya Kilimanjaro Marathon Company Limited.

Amesema muamko ni mkubwa na wanatarajia pia kuendelea kuuza tiketi kwa ajili yam bio za Grand Malt KM 5 huku usajili kwa ajili ya Kilimanjaro Premium Lager Km 42 na Tigo Kili International Half Marathon ukiwa umefungwa baada ya idadi ya washiriki kutimia mapema mwezi huu.

Ameongeza kuwa,  baada ya Dar es Salaam, zoezi hilo litahamia mkoani Arusha katika hoteli ya Kibo Palace Februari  21 na 22 kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni.

“Kituo cha mwisho ni Moshi Mjini ambapo zoezi hilo litafanyika Februari 23 (saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni), Februari 24 (kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni) na Februari 25 (kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni) katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU"), amesema

Katika hatua nyingine Waandaaji wa mbio hizo wameendelea kusisitiza kuhusu hatua zitakazochukuliwa dhidi ya watu wanaodaiwa kuuza tiketi mtandaoni kwa njia isiyo halali. “Watu hawa watachukuliwa hatua za kisheria kwa sababu ni marufuku kuuza tiketi bila idhini ya waandaaji na hata hivyo usajili umeshafungwa,” amesema

Watakaokimbia na namba feki zikiwemo za miaka iliyopita pia watachukuliwa hatua ikiwemo kuondolewa mashindanoni, kufutiwa matokeo na pia kufungiwa kushiriki katika Kilimanjaro Marathon kabisa.

Wadhamini wa mbio hii ni pamoja na Kilimanjaro Premium Lager-42km (Mdhamini Mkuu), Tigo- 21km Half Marathon, Grand Malt – 5Km Fun Run, wadhamini wa meza za majiTPC Sugar, Simba Cement, Kilimanjaro Water, TotalEnergies na wasambazaji maalumu Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles, KK Security na Keys Hotel.

Mbio hizi zinaandaliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions Limited.
Washiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon wakichukua namba zao za kpukimbilia katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Mjini Moshi Jumapili ijayo.

Washiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon wakiwa na furaha baada ya kupokea namba zao za kukimbilia katika viwanja vya Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zinatarajiwa  kufanyika Mjini Moshi Jumapili ijayo.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini