Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Kuelekea kwenye mchezo wao wa pili wa wa Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, mchezo wa Kundi D dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi amesema kuwa atamkosa Kiungo wa timu hiyo, Salum Abubakari (Sure Boy) kutokana na kuuguza Mtoto wake.
Kocha Nabi amesema Sure Boy ana matatizo ya kifamilia (Mtoto wake anafanyiwa upasuaji) hivyo hatokuwa kwenye mipango yake katika mchezo huo wa pili dhidi ya miamba ya soka kutoka nchini DR Congo, TP Mazembe, mchezo utakaopigwa Februari 19, 2023 kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Mchezo Wetu dhidi ya TP Mazembe, tutawakosa Bernard Morrison ambaye bado hajapona majeruhi yake tangu alipoumia kwenye mchezo wetu wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, lakini kwa Sure Boy atakosekana kwa sababu Mtoto wake ni magonjwa na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji,” amesema Kocha Nabi.
Hata hivyo, Kocha Nabi amesema huenda wakamkosa Mchezaji wao, Stephane Aziz Ki kwenye mchezo huo dhidi ya Mazembe kwa sababu ya hakufanya mazoezi na timu hiyo wakati wa maandalizi kabambe na timu hiyo kwenye mchezo huo muhimu kwao.
“Aziz Ki tunaweza kumkosa kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Mazembe lakini tutamuangalia kwenye ‘program’ ya leo ya mazoezi yetu kabla ya mchezo wa kesho, kama anaweza kuanza au asianze,” ameeleza Kocha Nabi.
Kuhusu Mlinzi, Mamadou Doumbia, Kocha Nabi amesema Mlinzi huyo hajasajiliwa kucheza Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika pekee bali amesajiliwa kuitumikia Yanga SC katika mashindano yote ambayo Klabu hiyo inashiriki.
“Mamadou kusajiliwa kwa muda mfupi sana, lakini kwa sasa tunaangalia apate muunganiko na Wachezaji wenzake Kikosini, akipata muunganiko atacheza na atatusaidia ni Mchezaji mzuri,” amesema.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments