MADEREVA WA MBIO ZA MAGARI WALIA NA WADHAMINI | ZamotoHabari

 Na.Khadija Seif, Michuzi blog

MADEREVA wa Mashindano ya mbio za magari ( Rally) wameomba wadau mbalimbali wa michezo kutoa ushirikiano katika kuupa sapoti mchezo huo kama wanavyotoa kwa michezo mingine kutokana na changamoto kubwa wanazokumbana nazo wakati wa maandalizi ya mashindano hayo  kimataifa.

Akizungumza na Wanahabari Leo Mei 20,2023 wakati wa Ufunguzi wa mafunzo ya siku 2 kwa madereva,waongozaji wa mchezo wa Mashindano ya mbio za magari Afisa Michezo kutoka Baraza la michezo nchini (BMT) Nicholaus Mihayo amesema Mchezo wa mashindano ya magari ni mchezo unaokuwa kwa kasi hivyo mafunzo hayo yanaenda kuangalia waendeshaji na waongozaji wa magari namna ya kuendesha kwa usalama .

"Wametazama namna ya vifaa vyako vya dereva,mfumo wa chombo unachoendesha ili kusitokee ajali zisizo za lazima kutokana na mchezo huo kuwa wa hatari. "

Hata Mihayo ameongeza kuwa wana imani na mafunzo hayo yaliyotolewa na wakufunzi kutoka nchini Afrika kusini yataenda kuongeza maarifa kwa watu hao na kukuza mchezo huo na kushiriki mashindano ya kimataifa.

Pia ametoa wito kwa Mashirikisho na vyama vya michezo kuwa milango ya Serikali ipo wazi kusikiliza changamoto na maboresha katika kuhakikisha michezo yote nchini inakua sehemu ya ajira ya kudumu.

Mwenyekiti wa Chama cha Mashindano ya Magari (AAT) Satinder birid amesema  kupitia msaada wa Shirikisho la mashindano ya mbio za magari (FIA) pamoja na chama cha Mbio za magari (AAT) wameshirikiana kuhakikisha Madereva wanapata mafunzo kwa mara ya kwanza kupitia vyama vyao kutoka mikoa 4 dar,Arusha, Iringa pamoja na Tanga.

" Mafunzo haya wamedhaminiwa na Shirikisho la Mbio za magari (FIA) ambapo wameona kimsingi kuna baadhi ya maeneo madereva, waongozaji wanapaswa kuongeza ujuzi ili kuboresha mchezo huo na kuongeza hamasa zaidi ya wadau kuvutiwa nao."

Pia amesema ni matumaini ya Serikali kuunga mkono mchezo huo ili mchezo huo utambulike nje na ndani ya nchi na kuzalisha watu wengi maarufu ambao pia watapata kipato kupitia mchezo huo.

Aidha amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kufungwa rasmi Mei 21,2023 ili kuwapa nafasi washiriki wa mafunzo hayo kuyafanyia kazi yale waliwasilisha katika mafunzo hayo.

Kwa upande wake mmoja wa mnufaika wa mafunzo hayo ya siku 2 kwa mchezo wa mbio za magari ambae ni dereva

Sultan chana  kutoka Mkoa wa Iringa ameeleza Kwa namna mafunzo hayo yameongeza ujuzi na maarifa ambayo yataenda kuleta hamasa ya mchezo huo kuwa na mashabiki na wadau kuunga mkono kama michezo mengine.

"Mafunzo niliyopata leo ni pamoja na jinsi ya kufunga mikanda uwapo katika  gari la mashindano,kutumia kifaa cha kuzima moto,kulihudumia gari kabla na baada ya mashindano. "

Hata hivyo amewaomba wadau wa mchezo huo kujitokeza kudhamini mashindano hayo kutokana na Madereva kupata changamoto ya maandalizi ya mashindano hayo .


Mwenyekiti wa Chama cha mbio za Magari (AAT) Satinder birid akizungumza na Wanahabari Leo Mei 20,2023 Jijini Dar es na kuwaomba wadau wajitokeze kusapoti mchezo wa mbio za magari ili kuendelea kuleta hamasa kwa wachezaji
Afisa Michezo kutoka Baraza la Michezo nchini (BMT) Nicholaus Mihayo akizungumza na Wanahabari na washiriki wa Mafunzo ya Usalama barabarani kwa Madereva na waongozaji wa Mbio za magari Leo Mei 20,2023 Jijini Dar es salaam na kueleza dhamira ya dhati kwa Serikali kuwa wataendelea kutoa ushirikiano kwenye michezo yote nchini inayotambulika na Baraza la michezo nchini.
Baadhi ya Madereva na waongozaji wa mbio za magari wakisikiliza mafunzo kutoka kwa wakufunzi kutokea nchini Afrika kusini ambao wataendesha mafunzo hayo  kwa siku 2 mfululizo Jijini Dar es salaam


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini