KANUNI ZAIBEBA USM ALGER KUWA MABINGWA CAFCC | ZamotoHabari

 NA EMMANUEL MBATILO MICHUZI TV

KLABU ya Yanga imeshindwa kuwa mabingwa licha kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya USM Algers kwenye mchezo wa Fainali kombe la Shirikisho mkondo wa pili mara baada ya matokeo  ya kwanza akiwanyumbani kuruhusu kufungwa mabao  2-1.

Katika mchezohuo ambao ulijaa vitimbwi mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa USM Algers hasa kuwasha mafataki na kusababisha moshi mwingi kujaa uwanjani na kufanya mpira kusimama mara kadhaa kwenye mchezo huo.

Yanga Sc ilianza kupata bao kupitia  kwa beki wao Djuma Shabaan kwa mkwaju wa penati dakika za mwanzo kipindi cha kwanza, bao ambalo liliweza kudumu mpaka dakika 90 ya mchezo.

Fiston Kalala Mayele amefanikiwa kuchukua kiatu cha ufungaji bora kwenye michuano hiyo kwa kufanikiwa kuwa kinara wa upachikaji wa mabao baada ya kupachika  mabao 7 kwenye michuano hiyo ambayo imefikia tamati leo.



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini