PROMOTA SEMUNYU: DULLA MBABE NGUMI TANZANIA INAMDAI TUMUUNGE MKONO AMALIZANE NA KATOMPA  | ZamotoHabari

Na.Khadija Seif,Michuzi TV

MKUZAJI Wa Ngumi za Kulipwa nchini Meja Selemani Semunyu amesema wakati vipaji vingine vya Mabondia vikiendelea kuibuliwa bondia Abdallah Pazi a.k.a Dulla Mbabe bado Mchezo unamuhitaji kwa Afya ya mchezo Huo na kuendelea kuleta Hamasa zaidi.

Akizungumza wakati akifanya Mahojiana kupitia Azam tv kipindi cha Michezo Meja Semunyu amesema kwa sasa Dulla Mbabe anaendelea na maandalizi na ameweka Kambi kwa Kocha Master Kinyogori ambae anasifika kwa ngumi za mahesabu.

Ameongeza kuwa Dulla Mbabe anahitajija kuendelea kuleta radha ya mchezo huo kutokana na mabondia wengine wanamtumia kama mfano Na sababu ya wao kuingia Kwenye Mchezo wa Masumbwi nchini.

Kuhusu Ugumu Wa Mechi amesema pambano Liko 50 Kwa 50 lakini kutokana Na hii mechi Ni muhimu Kwa Dula Ina nafasi kubwa Kwa Sababu amesoma mapungufu hasira za kupoteza Na akiongezea Na ufundi Wa Mwalimu kinyogoli Dula ana nafasi nzuri.

"Katompa ni bondia mzuri anapanga Ngumi wakati Dula anataka tupigane lakini kwa aina ya uchezaji Wa bondia kama huyo Dulla mbabe licha ya mchezo Wa kupenda kupigana inamuhitaji sana acheze ngumi za mahesabu kidogo nafikiri ndio maana yupo Kwa Kinyogoli ili kumkabili mpinzani huyo Julai 15,2023 Jijini Dar es salaam.

Semunyu amefafanua kuwa kabla ya pambano hilo yameandaliwa Mapambano Ya kutafuta "Champion wa Kitaa" lengo hasa kusaka vipaji kupitia Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam.

Ameongeza kuwa mabondia watakaofanya vizuri Katika mapambano hayo watapata nafasi ya kucheza Pambano kubwa la "Pay back Night 2023" kumsindikiza dulla Mbabe dhidi ya Mkongoman Eric Katompa.

Pia amewaomba Watanzania kumuunga Mkono dulla mbabe kuelekea pambano hilo huku akiongeza kuwa Pambano hilo la marejeo dulla mbabe atawapa faraja Watanzania wenye mapenzi na mchezo wa Masumbwi wakimuunga mkono.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini