Na Khadija Seif,Michuziblog
KAMPUNI ya Bongo Boxing Fighting (BFC) imeandaa mapambano 14 ya ngumi aina ya MuayThai (Ngumi za Thai) yatakayochezwa Julai 29, mwaka huu katika Ukumbi wa Superdom Masaki, Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari Promota wa mapambano hayo Mtendaji Mkuu wa The Superdome, Scott Patrick ameseema kuwa kutakuwa na pambano kuu litakalomshirikisha bondia Abdul Ubaya dhidi ya bondia kutoka Uganda Ivan Mgumba watakaowania Mkanda wa Dunia wa WBC.
Patrick amefafanua kuwa kutakuwa na pambano moja la Wanawake ambapo bondia Feriche Mashauri atapambana dhidi ya bondia kutoka Chiedza Homakoma kutoka Zimbabwe.
Pia amesema wataendelea kuendeleza mchezo wa Masumbwi nchini kuhakikisha mabondia wanatimiza ndoto zao na wanaongeza kipato chao kupitia vipaji vyao.
Nae Meneja Masoko wa Startimes Media, David Malisa ameeleza namna kampuni hiyo ilivyojipanga kurusha maudhui yote kuanzia kupima uzito pamoja na siku ya pambano lenyewe .
Malisa amesema wameshirikiana na BFC kuendeleza mchezo huo na mingine ijayo ikiwemo kickboxing ili kuendelea kuinua vipaji vya wachezaji wa mchezo huo.
"Wengi waliokuwa wateja wetu walitamani kuona mchezo wa ngumi, niwaambie wakae mkao wa kula, Jumamosi ijayo itakuwa ‘live’ kupitia chanel yetu ya Tv3 itaonesha pambano hilo na mengine yajayo naamini mtafurahia."
Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni Emanuel Shija dhidi ya Yusuph Fundi, Mbaraka Mtange dhidi ya Paul Owen, Abdulrazaki Kazumari dhidi ya Emanuel Patrick, Mwingereza Tomiwa Akindele dhidi ya Johnson Kihegula, Imani Matendo dhidi ya Frank Epimaki na wengine.
Pia, Musa Said dhidi ya Mkenya Amos Lion, mwandaaji wa ngumi hizo, Scott Farrel dhidi ya Marcus Warry, Fariche Joseph dhidi ya Mzimbabwe, Chiedza Homakoma na Hamis Msondo dhidi ya Ajemi Amani.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza machache namna kampuni hiyo ilivyojipanga kurusha maudhui ya kimichezo hasa mchezo wa Masumbwi 2023 na watazamaji watarajie kuona maudhui yote mubashara tv3
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments