Na BAKARI MADJESHI, Michuzi TV
Winga raia wa Msumbiji, LuÃs José Miquissone rasmi amerejea kwenye Kikosi cha Simba SC, amesajiliwa Kikosi hapo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Abha FC ya Saudi Arabia alipokuwa kwa mkopo wakati akiwa na Al Ahly SC ya Misri.
Simba SC imetangaza kumrejesha Miquissone Kikosini ikiwa na lengo la kuboresha Kikosi hicho ambacho kilikosa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kwa misimu miwili mfululizo.
LuÃs Miquissone amerejea Simba SC msimu huu wa 2023-2024, aliondoka na kusajiliwa na Al Ahly SC mwaka 2021 ambapo baada ya usajili huo Al Ahly walimtoa kwa mkopo katika Klabu ya Abha ya Saudi Arabia.
Miquissone amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili na uwezekano wa kuongeza mkataba mwengine Kikosini hapo Msimbazi.
Hadi sasa Simba SC imesajili wachezaji Willy Essomba Onana kutoka Rayon Sports ya Rwanda, Aubin Kramo Koume kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast, Mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone kutoka Klabu ya Coton Sports ya Cameroon, Fabrice Ngoma kutoka Al Hilal ya Sudan.
Wachezaji wa ndani walisajliwa hadi sasa ni Hussein Kazi, Abdallah Hamis na Shaaban Iddi Chilunda.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments