EEEH DE GEA APEWA THANK YOU MAN UNITED !!! | ZamotoHabari


Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Ni rasmi Manchester United ya Uingereza imetangaza kuachana na Golikipa wake namba moja, raia wa Hispania, David De Gea kuelekea msimu ujao wa mashindano wa 2023-2024.

De Gea ameachwa na Manchester United, alitua Kikosini hapo akitokea
Atletico Madrid, mwaka 2011, De Gea amedumu Kikosini hapo kwa miaka 12 na alikuwa miongoni mwa Magolikipa bora kuwahi kutokea Man United.

De Gea ameondoka Man United akiwa amecheza michezo 545, akiwa na michezo 190 ambayo hajaruhusu bao (clean sheet).

Kupitia kurasa zake zake za mitandao ya kijamii, David De Gea ameandika: “Nawaaga mashabiki wote wa Manchester United, nashindwa kuandika ujumbe huu!!!.”

“Nawashukuru wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka 12 nilipokuwa hapa, Man United, tumeshinda mengi tangu alipokuwa Sir Alex Ferguson ambaye alinileta hapa na kunipa nafasi Kikosini. Ni fahari kwangu kucheza kwenye Klabu hii kubwa na maarufu duniani.”

Hata hivyo, Manchester United imehusishwa kumsajili Golikipa wa Kimataifa wa Cameroon, André Onana.


 

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini