GBT YATWAA TUZO YA MAMLAKA BORA YA USIMAMIZI (REGULATORY BOARD) | ZamotoHabari

 

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

BODI ya Usimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board of Tanzania, GBT) imefanikiwa kutwaa TUZO ya mshindi wa kwanza (First winner prize) katika kundi la Mamlaka za Usimamizi (Regulatory Bodies) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofikia kilele Julai 13, 2023.

TanTrade iliweka utaratibu mpya wa namna ya kumpata mshindi ambapo mwaka huu wananchi ndio waliopewa fursa ya kuchagua mshindi kwa kupiga kura kupitia mtandao tofauti na miaka ya nyuma ambapo kamati maalum ilikuwa ikipita kwenye mabanda kisha kuchagua washindi.

“Sisi tunachukulia haya ni mafanikio makubwa sana kwetu na tunawashukuru Watanzania kwa kututambau na kuthamini kazi nzuri inayofanywa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania GBT.” Alisema Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Alisema Wananchi wanatambua mchango wa sekta ya michezo katika maendeleo ya nchi.

“Katika mwaka huu w afedha ulioshia Juni 2023 kiasi cha shilingi bilioni 160 za kodi ya moja kwa moja zitakusanywa kutoka kwenye sekta ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi bilioni 148 zilizokusanywa katika mwaka wa fedha uliopita 2022.” Alifafanua.

Alisema GBT itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo. “Michezo ya kubahatisha ni burudani sio ajira, ni ajira kwa waendeshaji lakini ni burudani kwa wachezaji.” Aliwaasa washiriki wa michezo ya kubahatisha.

Alisema GBT imefikisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na kadiri muda unavyokwenda ndivyo imekuwa ikiimarika zaidi.

Aidha akifafanua zaidi kuhusu tuzo, Afisa Uhusiano Mwandamizi GBT, Zena Athumani amesema mbali na kupata tuzo hiyo ya mshindi wa kwanza kundi la Mamlaka za Usimamizi, GBT pia ilitwaa tuzo ya mshindi wa tatu wa Banda bora la Maonesho mwaka huu.


Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe akionyesha tuzo hiyo



Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe akionyesha tuzo hiyo na ile ya mshindi wa tatu ya banda bora.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi GBT, Balozi (mstaafu) Moset Jonathan Mello (katika) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi hiyo walipotembelea banda la GBT Sabnasaba.



Mkurugenzi Mkuu GBT, Bw. James Mbalwe (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya GBT iliyokuwa ikitoa huduma Sabasaba



Balozi mstaafu Mello, akiwa katika picha ya pamoja na Waendeshaji wa michezo ya kubahatisha



Balozi mstaafu Mello, akiwa katika picha ya pamoja na Waendeshaji wa michezo ya kubahatisha



Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini