… MAYELE HUYOOO, INASUBIRIWA ‘THANK YOU’ | ZamotoHabari

 

TETESI za soka nchini zinadai kuwa Mshambuliaji raia wa DR Congo, Fiston Kalala Mayele anaondoka Young Africans SC na imedaiwa kuwa anaondoka Kikosini hapo ili kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine.

Imeripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kupitia kwa Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya soka nchini wamenukuliwa wakichapisha taarifa hizo za Nyota huyo kuondoka katika viunga vya mitaa ya Twiga na Jangwani.

Hata hivyo, tetesi hizo zinadai kuwa Mshambuliaji huyo mahiri kwa upachikaji wa mabao, ametajwa kutimkia katika Klabu ya Pyramids ya Misri (bado haijathibitishwa rasmi) msimu ujao wa mashindano.

Mayele, msimu uliopita wa 2022-2023 alifanikiwa kuweka kambani mabao 17 akifungana na Mshambuliaji wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza wote wakipewa Kiatu hicho baada ya kufungana kwa mabao hayo.

Msimu wa 2021-2022, Mayele alikosa Kiatu cha Dhahabu baada ya kuzidiwa bao moja pekee na aliyekuwa Mshambuliaji wa Geita Gold FC, George Mpole. Mayele alifunga mabao 16 huku Mpole akifunga mabao 17 na kuibuka Mfungaji bora wa msimu huo wa 2021-2022.

Fiston Mayele alijiunga na Young Africans SC, Agosti 01, 2021 akitokea AS Vita Club ya DR Congo, Mayele alisajiliwa Yanga SC kwa mkataba wa miaka miwili na alikuwa Mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa kwenye msimu huo wa mashindano kwenye Klabu hiyo ya Yanga.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini