Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Mwanariadha kutoka nchini Marekani, Alysia Montaño (37) amekimbia na kumaliza mbio za mita 800 akiwa na ujauzito wa miezi mitano katika mbio za US Track, Field national.
Mwanamama huyo amemaliza mbio hizo, kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Mtandao wa michezo nchini Ghana, GTV Sports mapema Julai 5, 2023.
Hata hivyo, si mara ya kwanza kwa Montaño kumaliza mbio akiwa mjamzito, aliwahi kuushangaza umma kwa kufanya hivyo mwaka 2014, mwezi Juni akiwa na ujauzito wa miezi nane na nusu (wiki 34) katika mbio za USATF's USA Outdoor Track, Field Championships.
Baada ya kumaliza mbio hizo akiwa na hali hiyo, Montaño aliliambia jarida la CBS LA: “Najua kuna unyanyapaa, lakini hii ni nzuri kwa afya ya Mama na Mtoto.”
Vile vile alisema alitarajia mtoto wake wa kwanza, pia aliliambia Jarida la Associated Press kwamba amekuwa akikimbia katika kipindi chote cha ujauzito. Yeye na mume wake, Louis Montaño walipanga kupata mtoto kwenye ‘mwaka wa mbali’ ili aweze kushiriki katika mashindano ya dunia na Olimpiki, kulingana na taarifa iliyoripotiwa na CBS LA.
Agosti 15, 2014, alijifungua mtoto wake wa kwanza, Linnea Dori Montaño na mwaka uliofuata wa 2015 alishinda mbio za Mita 800 kama kawaida yake katika Fainali za US Trials na kufuzu mashindano ya dunia mjini Beijing nchini China mwaka huo wa 2015.
Alysia Montaño ni bingwa mara sita wa mbio hizo za Mita 800 za ‘USA Outdoor Track and Field Championships’, ameshinda ubingwa huo mwaka 2007, 2010, 2011, 2012, 2013 na 2015.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments