Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Wachezaji watatu wa Al Hilal SC ya Sudan, Fabrice Ngoma, Ibrahim Imoro na Lamin Jarjou wameshutumiwa na Klabu hiyo kuvunja mikataba yao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mitandao ya kijamii ya Klabu hiyo, imeeleza kuwa wachezaji hao wamevunja mikataba hiyo bila taratibu na wote watachukuliwa hatua za kisheria.
“Wachezaji wetu, Fabrice Ngoma, Ibrahim Imoro na Lamin Jarjou wamevunja mikataba yao bila sababu. Hatukubaliani na hilo, tutaanza kuwachukulia hatua za kisheria dhidi yao,” imeeleza taarifa ya Klabu hiyo.
Kiungo raia wa DR Congo, Fabrice Ngoma, amehusishwa kusajiliwa na Klabu ya Simba ya Tanzania wakati Mshambuliaji Lamin Jarjou na Mlinzi wa pembeni (kushoto) kutoka Ghana, Ibrahim Imoro haijafahamika wapi wanaelekea.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments