Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Young Africans SC wamedhihirisha kuwa msimu ujao wa mashindano wa 2023-2024 hawatatetema tena kama ilivyokuwa kwenye msimu miwili iliyopita wakati wakiwa na Mshambuliaji wao raia wa DR Congo, Fiston Kalala Mayele.
Mayele hakuwa kwenye orodha ya wachezaji waliotambulishwa kwenye Kikosi hicho cha Wananchi cha msimu ujao ambacho kimetangazwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi.
Fiston Mayele sanjari na wachezaji wengine kutoka DR Congo, Yannick Bangala na Djuma Shabani (Sojaa ya Bemba) hawakuwepo kabisa kwenye dimba la Mkapa wakati Maulid Kitenge na Zembwela wakitaja orodha ya wachezaji hao watakaounda Kikosi cha Wananchi msimu unaofuata.
Wachezaji wapya wa kigeni waliotambulishwa na Yanga SC ni Mahlatse Makudubela (Skudu) kutoka Afrika Kusini, raia wa Ivory Coast, Pacôme Zouzoua, Kouassi Attohoula Yao, Gift Fred kutoka Uganda na Maxi Mpia Nzengeli kutoka DR Congo. Wachezaji wengine wa ndani (Tanzania) ni Jonas Mkude na Nickson Kibabage.
Kikosi cha Yanga SC msimu ujao kina wachezaji, Makipa, Djigui Diarra, Metacha Mnata, Walinzi ni Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Joyce Lomalisa, Kibwana Shomari.
Viungo ni Zawadi Mauya, Mudathir Yahya, Farid Mussa, Salum Abubakari (Sure Boy), Khalid Aucho na Stephane Aziz Ki. Washambuliaji ni Kennedy Musonda, Crispin Ngushi, Dennis Nkane, Jesus Moloko na Clement Mzize.
Pia katika katika kusheherekia wiki ya Mwananchi, Yanga imecheza mechi ya Kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na Kennedy Musonda dakika ya 45-1 kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka kwa nyota wao mpya Max Nzengeli.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments