Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League jana iliipamba mechi kati ya Azam FC na Simba SC maarufu kama ‘Mzizima Derby’ kwa kuandaa matukio kadhaa ikiwemo kukabidhi zawadi ya tuzo na pesa taslimu kwa mchezaji na kocha bora wa ligi hiyo kwa mwezi Agosti.
Mechi hiyo ilifanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na kuisha kwa timu ya Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 2-0. Wateja mbalimbali wa benki ya NBC walipata fursa ya kuutazama mchezo huo wakiwa katika jukwaa la VIP kupitia udhamini wa benki hiyo.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Abdul Karim Mkila aliiwakilisha benki hiyo katika kukabidhi tuzo na hundi ya fedha yenye thamani ya sh milioni moja, kwa mchezaji bora mwezi Agosti, ambae ni kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua huku Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya akikabidhi zawadi kama hizo kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids ambae aliiibuka kocha bora kwa mwezi huo.
Katika mchezo huo wa jana ilishuhudiwa kipa wa Simba SC, Moussa Camara akiibuka mchezaji bora wa mchezo huo na kukabidhiwa zawadi ya tuzo kutoka benki hiyo.
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Abdul Karim Mkila (Kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua alietangazwa mchezi bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agosti wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids alietangazwa kocha wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agostii wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Dar Es Salaam (DRFA) Lameck Nyambaya (Kushoto) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa kocha mkuu wa klabu ya SC Fadlu Davids alietangazwa kocha wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agostii wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,
Meneja wa maendeleo ya biashara wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Obedy Ngavatula (Kulia) akikabidhi tuzo ya mchezaji bora kwa kipa wa Simba SC, Moussa Camara alieibuka mchezaji bora wa mchezo kati ya Azam FC na Simba SC uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,
Kipa wa Simba SC, Moussa Camara akifurahia na tuzo yake baada ya kuibuka mchezaji bora wa mchezo kati ya Azam FC na Simba SC uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,
Meneja wa Benki ya NBC tawi la Zanzibar Bw Abdul Karim Mkila (Kushoto) akikabidhi tuzo kwa kiungo wa Simba SC, Jean Charles Ahoua alietangazwa mchezi bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Agosti wakati wa mechi kati ya Azam FC na Simba SC iliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana. Klabu ya Simba SC iliibuka na ushindi wa goli 2-0,
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jana ilishuhudiwa Klabu ya Simba SC ikiibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Azam FC
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments