Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Wajasiriamali wadogowadogo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara, wameshukuru uwepo wa michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara, Wakala za Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali mkoani Morogoro, kwa kuwa imewaongezea vipato vyao.
Kiongozi na Mwamuzi wa zamani wa mchezo wa mpira wa netiboli, Mwajuma Kisengo aliyetokea Jijini Dar es Salaam akiwa na biashara ya nguo za michezo amesema michezo hiyo imetoa fursa ya wajasiriamali kujiongeza na kuleta bidhaa mbalimbali za kuwauzia wachezaji wanaoshiriki kwenye mchezo hiyo
Naye Hope Chinga kutoka jijini Dodoma akiwa anauza juisi za tende, matunda na lishe kwa ajili ya wenye matatizo ya kiafya, ambazo anawauzia wanamichezo wanaoshiriki SHIMIWI 2024, inawaongezea kipato na kujikimu kimaisha.
Kwa upande wake Samwel Kahabuka kutoka Mwanza naye ameishukuru serikali kwa kufanya michezo kwa watumishi wa umma kwani inasaidia kuimarisha afya zao, na ni ajira, na pia kuwasaidia wajasiriamali wadogowadogo kuongeza kipato chao.
Naye Hadija Kihonda mkazi wa Morogoro anayeuza marashi kutoka Dubai ameshukuru maamuzi ya mkoa wa Morogoro kuwa mwenyeji wa michezo hiyo, maana kumewezesha wajasiriamali kuuza bidhaa mbalimbali.
Pia kwa nyakati tofauti Moses Mrisho muuza madafu mkazi wa Morogoro, naye Fortunatus Felician muuza batiki wa Jiji la Dar es Salaam na Pendo Florian mkazi wa Morogoro anayeuza uji wa ulezi, mhogo na mchele wameshukuru uwepo wa SHIMIWI.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments