Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amewataka wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar Herous, kucheza kizalendo na kufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi wao.
Ameyasema hayo katika Chuo Kikuu cha Sumait Chukwani Wilaya Magharibi ‘B’ wakati alipowatembelea wachezaji wa Timu hiyo amesema ni vyema wachezaji wakiwa na malengo mahsusi ambayo yatawasaidia kucheza kwa murari na hamasa kubwa ili kufikia mafanikio ya ushindi.
Waziri Tabia amewaombe dua ya mafanikio vijana hao ili kombe libaki Zanzibar na imani yake kwamba vijana hao wanauwezo mkubwa wa kuonyesha vipaji vyao katika uchezaji wa mpira wa miguu.
Aidha amesema fedha zitatolewa kwa mshindi wa shindano hilo na kuahidi kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Mwinyi kwa kununua magoli katika shindano hilo .
Nae Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Zanzibar Herous Hemed Sleiman Morocco amesema ameridhishwa na ujio wa Mhe, Waziri wa Habari na kuelezea jinsi walivyojipanga imara katika mapambano ya kuwania Kombe la Mapinduzi 2025.
Amesema ujio huo umewapa nguvu vijana hao na kuengeza murali katika mchuano huo ili kuhakikisha lengo lao la ushindi linatimia.
‘’Nipelekee salamu kwa Mhe.Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kwamba tunakwenda kupambana kwa mwisho wa uwezo wetu kwa kila hatua na mafaniko. ‘’ amesema Kocha Hemed.
Kwa upande wa Kapteni wa Timu ya Taifa , Zanzibar Heroes Ahmed Ali Suleiman akizungumza kwa niaba ya wenzake ameiahidi Serikali pamoja na Wazanzibar wote kuhakikisha wanapambana ili kuipatia heshima nchi yao.
‘Tunajipanga vyema katika kuhakikisha tunashinda, Kombe la Mapinduzi linabaki nchini kwetu’’ amesema Kocha Ahmed.
Akitoa shukrani kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe Dk Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada zao kwa kuwajali na kutoa mashirikiano yao, kabla ya ligi kuanza jambo ambalo limewatia moyo wachezaji wao.
Imetolewa na Kitengo cha Habari Mawasiliano na Uhusiano.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments