
Leo tarehe 12 Aprili, Uwanja wa Selhurst Park utashuhudia pambano kali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati ya Crystal Palace na Newcastle United majira ya saa 16:00. Mechi hii ina umuhimu mkubwa kwa timu zote mbili, kwani zinatofautiana alama tatu tu kwenye msimamo
Newcastle United iko nafasi ya 12 na pointi 42 baada ya kucheza mechi 31, huku Crystal Palace ikiwa nafasi ya 14 na pointi 39 baada ya mechi 30. Kwa hivyo, Palace ana mechi moja mkononi, na ushindi leo unaweza kuwafanya wapite Newcastle kwenye msimamo. Mwamuzi Andrew Madley ndiye atakayesimamia sheria 17, jambo linaloongeza changamoto kwa wachezji kudhibiti nidhamu.
Crystal Palace wana majeruhi watatu muhimu Cheick Doucoure, Eddie Nketiah, na Caleb Kporha. Kutokuwepo kwa Doucoure kwenye kiungo cha kati kunaweza kudhoofisha mipira ya kukaba na usambazaji wa mpira. Nketiah, aliyekuwa akitarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji, pia hayupo. Kwa upande mwingine.
Newcastle wana majeruhi watano wakubwa Bruno Guimaraes, Lewis Miley, Fabian Schar, Emil Krafth, na Sven Botman. Hasara ya Guimaraes na Schar ni pigo kubwa kwa moyo wa uwanja na safu ya ulinzi wa Newcastle, jambo linaloweza kufanya timu hiyo iwe tete zaidi, hasa ugenini.
Crystal Palace wameshinda mechi 10, sare 9, na kushindwa 11 msimu huu. Hii inaonyesha timu yenye uthabiti wa kati lakini inayoweza kusumbua wapinzani wakati wa nyumbani. Newcastle wamebora kidogo kwa ushindi 12, sare 6, na kupoteza 13 lakini tofauti ni ndogo.
Mara ya mwisho timu hizi mbili zikakutana kwenye raundi ya kwanza ya EPL msimu huu, Newcastle United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Ushindi huo utawapa kujiamini, ingawa sasa wako ugenini na hawana wachezaji wao muhimu. Jisajili sasa
Crystal Palace, kwa upande wao, watakuwa na nia ya kulipiza kisasi na kugeuza mwenendo wa michezo ya hivi karibuni. Selhurst Park ni uwanja gumu kwa wageni, na shabiki wa Palace wanajulikana kuwa wabishi, hivyo Newcastle wanapaswa kuwa makini.
Kocha Oliver Glasner wa Crystal Palace anapenda kucheza mpira wa kukaba kwa nguvu kwenye kiungo na kushambulia kwa kasi. Akiwa na majeruhi wachache kwa kulinganisha na Newcastle, Glasner anaweza kutumia fursa hiyo kushambulia zaidi.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kwa upande wa Newcastle, Eddie Howe atalazimika kutumia wachezaji wa akiba kuziba mapengo ya Guimaraes na Schar. Uchezaji wao wa mpira unaweza kupungua kasi, wakitegemea zaidi mipira ya yakutenga na kutumia wachezaji wa pembeni.
Kutokuwepo kwa wachezaji wengi wa Newcastle kunaweza kusawazisha nguvu kwa Palace, hasa wakiwa nyumbani. Ingawa Newcastle alishinda mkutano wa kwanza, hali sasa ni tofauti. Crystal Palace ana nafasi nzuri ya kuchukua angalau pointi moja.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA



0 Comments