Leo Juni 5, 2026 saa 05:00 alfajiri, Uwanja wa Estadio Nemesio Diez (au Estadio Azteca) utakuwa jukwaa la mchezo wa kirafiki kati ya Mexico na Serbia.

Mexico wakiwa mmoja wa wenyeji wa Kombe la Dunia la 2026, wamepangwa Kundi A pamoja na Afrika Kusini, Korea Kusini na Jamhuri ya Cheki. Serbia kwa upande wao hawakufuzu kushiriki fainali hizo, walimaliza nafasi ya tatu katika Kundi K la kufuzu nyuma ya Albania.

Katika historia timu hizi zimekutana mara moja tu Novemba 2011, Mexico walishinda 2-0 kwa mabao ya Carlos Salcido na Javier Hernández. Hivyo, Mexico wana ubabe kamili wa ushindi katika rekodi hiyo. Mexico wanaendelea na rekodi nzuri ya kutofungwa katika mechi saba za mwaka 2026 (ushindi 5 na sare 2), wakiwa wamefunga mabao 10 na kufungwa bao 1 pekee.

Kocha Javier Aguirre ameitisha kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji waliokomaa na vijana wapya kwa Kombe la Dunia. Kipa Guillermo Ochoa anaongozana na Raúl Rangel na Carlos Acevedo, huku safu ya ulinzi ikiwa na Edson Álvarez, César Montes na Johan Vásquez. Raúl Jiménez ndiye tegemeo la ushambuliaji akisaidiwa na Santiago Gimenez, Alexis Vega na Julián Quiñones, huku kijana Gilberto Mora (17) akiwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuonesha uhodari wao.

Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa Serbia, kocha Veljko Paunovic ana changamoto kubwa ya wachezaji muhimu kutokuwepo. Strahinja Pavlović (AC Milan), Andrija Živković na wengine wamejitenga na kikosi kutokana na uchovu na majeruhi baada ya kichapo cha 3-0 kutoka Cape Verde. Serbia wameshindwa kushinda katika mechi za ugenini huku rekodi yao ya mwaka 2026 ikiwa ni ushindi 5 na kupoteza 5 kwenye mashindano yote. wachezaji wa kutegemewa zaidi katika safu ya ushambuliaji ni Aleksandar Mitrović na Dušan Vlahović. Jisajili

Wachambuzi wanatabiri ushindi kwa Mexico kutokana na ubora wa nyumbani, tofauti ya kiwango cha timu, na motisha ya Mexico ya kuingia Kombe la Dunia kwa kasi ya ushindi. Uwanja unatazamiwa kujaa mashabiki zaidi ya 30,000 wakiwapa moyo wachezaji wao kwenye mechi hii ya mwisho kabla ya kukutana na Afrika Kusini Juni 11. Serbia wakitumia fursa hii kujipima dhidi ya timu yenye nguvu licha ya kukosa tiketi ya kufuzu.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA