Tanzania yaombwa kujiunga na Ufaransa

JUMUIYA ya Kimataifa ya Nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa (OIF), imeiomba Tanzania kujiunga nayo ili kukuza demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu.

OIF inajumuisha nchi wanachama 84 duniani, huku asilimia 43 ya mataifa duniani yanatumia lugha ya kifaransa yenye watu wanaokadiriwa kufikia milioni 300, na nusu yao wanatokea nchi za Afrika.

Balozi wa Ufaransa nchini, Frederic Clavier aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya OIF itakayoanza kesho hadi Machi 25.

“Tupo tayari kuingia katika mazungumzo na serikali ya Tanzania katika maeneo wanayotaka tusaidie, pia tunaikaribisha Tanzania kuingia katika jumuiya yetu,” alisema Balozi Federic.

Alisema nchi wanachama wa IOF wamekuwa wakisaidia kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu nchini, hususani elimu ya chuo kikuu, kwa kuwasomesha wanafunzi wa Kitanzania katika nchi zao.

Akitolea mfano, Balozi Clavier alisema Ufaransa imekuwa mstari wa mbele katika kuwafadhili kimasomo Watanzania kwenda kusoma shahada na uzamili wa fani mbalimbali.

Balozi Clavier alisema ifikapo mwaka 2050 idadi ya watu watakaokuwa wanazungumza Kifaransa itafikia milioni 750.

Alisema OIF imedhamiria kuendeleza mshikamano na utamaduni wa kisiasa katika nchi mbalimbali duniani.Alisema lugha ya Kiswahili inazungumzwa na watu takribani milioni 100 duniani, hivyo mchanganyiko wa lugha hiyo na za kigeni pamoja na Kifaransa kutafungua milango ya ajira Tanzania na duniani.

Naye balozi wa Uswisi nchini, Florence Tinguely Mattli alisema mabalozi wa IOF wamedhamiria kuendeleza maadili na undugu uliodumu kwa miaka mingi.

Alisema usiku wa IOF utafunguliwa na Balozi wa Morocco nchini kwa kushirikiana na wawakilishi wote wa kibalozi wa Kifaransa nchini.

The post Tanzania yaombwa kujiunga na Ufaransa appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini