ZIKIWA zimebaki saa chache kulifikia Uzinduzi wa Tamasha la Wasafi Festival 2018 mkoani Mtwara, staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na timu nzima ya wsanii wote watakaokinukisha imewasili mkoani humo, jana Ijumaa, Novemba 22, 2018.
Wakiwa njiani kuelekea Mtwara, Diamond na Mameneja wake walijikuta wakishindwa kujizuia na kusimamisha msafara na kisha kufunga barabara kwa kucheza huku muigizaji Jacquline Wolper, wakipandwa na mizuka ya kufa mtu.
Tamasha la Wasafi Festival litafanyika Jumamosi ya Novemba 24, 2018 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, kwa wakazi wote wa Mtwara na mikoa ya Kusini.
Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika Tamasha hilo ambao wameongozana na Diamond ni Harmonize, Rayvanny, Dudu Baya, Country Boy, Lava Lava, Young Killer, Navy Kenzo, Chin Bees, Mbosso, Queen Darling, mchekeshaji Dulvan na wengine kibao.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments