Mwimbaji wa Bongofleva Vanessa Mdee amekutana na Rais wa kwanza Mwanamke Afrika Ellen Johnson-Sirleaf wa Liberia ambapo mbali ya Urais aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini na katika mashirika ya Kimataifa.
Uchaguzi wa Urais mwaka 2005 Liberia ulirudiwa baada Wagombea kutopata kura za kutosha ambapo kwenye round ya kwanza Ellen alikuwa wa pili, Katika raundi ya pili Ellen alitangazwa Mshindi ambapo hata hivyo George Weah alipeleka mashtaka Mahakama kuu akidai kuwa Uchaguzi haukuwa wa haki.
Mwaka 2016 Ellen mwenye umri wa miaka 80 alitajwa katika jarida la Forbes kwenye nafasi ya 83 katika orodha ya Wanawake wenye nguvu zaidi duniani.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments