Makubwa: Waziri Jafo Kuzindua Kampeni ya Wananchi Kutopeana Mikono


Waziri wa TAMISEMI kuzindua kampeni iitwayo 'Nakupenda, unanipenda, usinishike mkono' ili Watanzania waache kushikana mikononi

Jafo amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akitoa neno la shukrani kwa hotuba ya wakati akifunga semina ya siku 3 kwa maofisa afya wa Halmashauri na mikoa nchini

Ameeleza "Hii ni hatari sana hasa kwa viongozi, utakuta katika mkoa unaofanya ziara watu zaidi ya 40 wanakusubiri mnapeana mikono wakati kuna magonjwa ya kuambukiza, nataka tuwe tunapungiana mikono."

Tayari ameshazungumza na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ili waone namna bora ya kuliweka jambo hilo kwa faida ya Watanzania

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini