Mwanadada Rose Muhando ametangaza kurudi tena katika dini yake ya kiislamu baada ya kusema kuwa amegundua kuwa ule upendo aliwahi kuambiwa upo katika ukristo hauoni zaidi ya majonzi na maumivu kila siku.
Habari za Rose Muhando zimekuwa zikisambaa sana hapa karibuni kutokana kuwa mwanadada huyo kwa sasa amekuwa akinekana kama amechanganyikiwa sana na kuwa amefirisika na hata watoto wake hawana tena mahali pa kuishi.
Wakati ninaokoka niliambiwa maneno ya upendo sana na kwamba nitakutana na upendo lakini badalayake nimekuwa nikikutana na mahsuti tu kila siku, kwa mfano mtu anakuharika sehemu unashindwa kufika na unatoa taarifa lakini kesho yake unasikia kuwa anatangaza umemtapeli, wanashindwa kujua na kukumbuka hata jema moja kutoka kwangu.Nafikiria kurudi kwenye dini yangu ninaamini nitapata faraja.
Rose alikuwa moja ya wasanii wakubwa sana wa injili huku akisifia kila kona ya Tanzania na nje ya Tanzania kwa kazi zake, nyimbo zake zilikuwa zikipendwa na kila mtu bila kujali umri wala dini.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments