Azam FC Kuishusha Yanga Kibabe

Azam FC Kuishusha Yanga Kibabe
Baada ya Yanga kuwashusha kibabe Azam FC kileleni na kuendelea kujikita wakiwa na pointi 44 huku Azam wakiwa na pointi 40, uongozi wa Azam FC umesema unaitambua dawa itakayowasaidia kurejea kwenye nafasi ya kwanza.

Ofisa habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema wanatambua ushindani uliopo ligi Kuu na ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ni lazima wapate matokeo mazuri katika michezo yao.

"Kila baada ya kumaliza mchezo tunatambua kuna kazi mpya inakuja mbele yetu, kama ambavyo ipo kwa sasa, Yanga ni vinara nasi tunafuatia hivyo ili kuweza kurejea kwenye nafasi hiyo ni lazima tupate matokeo.

"Mchezo wetu ujao ni dhidi ya Mtibwa Sugar, tunawaheshimu wapinzani wetu na tutawafuata nyumbani kwao Morogoro, hesabu zetu ni kupata pointi tatu, wachezaji wameshaanza mazoezi ili kuweza kujijenga," alisema.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini