Kocha Simba Akitaja Kikosi Kitakachoivaa KMC Leo

Kocha Simba Akitaja Kikosi Kitakachoivaa KMC Leo
Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgjiji, Patrick Aussems, ameamua kuja na njia mbadala ya kuingamiza Nkana Red Devils ya Zambia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili hii.

Simba itakuwa inashuka dimbani kukipiga na mashetani hao ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya ule wa awamu ya kwanza kumalizika kwa kufungwa mabao 2-1 ugenini.

Kuelekea mechi na Nkana, Simba leo itakuwa na kibarua cha ligi kucheza na KMC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kipute cha leo na KMC kimefanya Mbelgiji Aussems kubadili aina ya wachezaji ambao atawatumia ili kuwapa nafasi wale nyota Jumapili dhidi ya Nkana.

Imeelezwa kuwa Mbelgiji atawatumia wachezaji wengi zaidi ambao hawachezi katika kikosi cha kwanza kwa hofu ya kutoumia kabla hawajakutana na miamba hiyo ya Zambia.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini