Siku chache zilizopita kuna taarifa zilisambaa kuwa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz amezidiwa kwa Mara nyingine na kurudishwa nchini Ujerumani kwa ajili ya matibabu.
Global Publishers wanaripoti kuwa baada ya Ommy Dimpoz kufanyiwa upasuaji wa awali wa koo hadi tumboni alipata tatizo la kujaa usaha ambalo ndilo lililomfanya azidiwe na familia ikalazimika kumpeleka Ujerumani baada ya kushauriwa kuwa kuna wataalam wazuri wa tatizo lake.
Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimvutia waya baba mzazi wa Dimpoz aliyeko Sumbawanga mkaoni Rukwa ambapo alipopatikana alithibitisha mwanaye kuzidiwa hivi karibuni na kwamba amepelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.
Ni kweli walinijulisha kwamba mwanangu amezidiwa tena, wakampeleka Ujerumani kwa ajili ya matibabu zaidi kisha kufanyiwa operesheni kwa mara nyingine na nimekuwa nikiwasiliana nao kujua hali yake.
Kikubwa kabisa niwaombe Watanzania wenzangu tumuombee Dimpoz, bado anaumwa yupo hospitalini, tumuombee aweze kuwa na afya njema”.
Lakini pia Gazeti hilo lilimsaka Meneja wa Ommy, Seven Mosha ambaye alifunguka kuwa Dimpoz kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu nchini humo na kwamba hali aliyokuwa nayo awali na sasa, ni vitu viwili tofauti, afya yake imeimarika maradufu na sasa anaweza kuongea vizuri kwani sauti inatoka.
Kwa sasa kwa kweli tunamshukuru Mungu yupo vizuri. Alivyoenda kule na alivyo sasa kwa kweli tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu, amepata ahueni kubwa”.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments