Petit Man Athibitisha Kuwa Hana Bifu na Familia Ya Esma

Petit Man Athibitisha Kuwa Hana Bifu na Familia Ya Esma
Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache amefunguka na kuweka wazi kuwa hana Bifu na familia ya aliyekuwa mke wake Esma Platnumz.

Petit amesema kuwa hata Baada ya kuachana na Esma Platnumz amekuwa hana tatizo na familia yake na ndio mama yeye na mkwe wake Mama Diamond bado wanaongea vizuri bila tatizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Mtandao wa Dizzim Online, Petit Man amefunguka haya:

Sina ugomvi wowote na familia ile, ndio maana hadi leo unaona mimi na mama tunaongea vizuri tunakomentiana vizuri kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi“.

Petit Man na Esma waliachana miezi michache iliyopita Baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka minne na kuzaa Mtoto mmoja pamoja.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini