JESHI la Wananchi Tanzania limesema liko tayari kutumia meli yake yenye uwezo wa kubeba tani 500 kusafirisha korosho hadi jijini Dar es Salaam baada ya maghala yaliyopo mkoani Mtwara kujaa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Wananchi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo katika kikao chake na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mtwara.
Amesema katika ziara yake aliyoifanya kwenye maghala makuu ameshuhudia korosho kujaa kwenye maghala hayo na kusema iwapo zitaendelea kukusanywa kwa wananchi jeshi litalazimika kutumia meli yake kupunguza sehemu ya zao hilo ili kuhifadhiwa Dar es Salaam.
Hata hivyo, amesema kuhusu upatikanaji wa maghala jijini Dar es Salaam jeshi litalazimika kufanya mazungumzo na wizara ya kilimo ili kuona namna ya kuandaa maghala hayo kwa ajili ya kutunzia korosho.
Kuhusu ubanguaji wake, Jenerali Mabeyo amesema vikundi vya wabanguaji wadogo watatumika kuzibangua na kwamba kiktu kikubwa kinachohitajika ni kuongezea nguvu-kazi ya watu ili kazi hiyo iweze kufanyika haraka na kwa tija.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments