Mwakyembe Aagiza 'Media' Kucheza Nyimbo za Dansi

Mwakyembe Aagiza 'Media' Kucheza Nyimbo za Dansi
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Mh. Harrison Mwakyembe, ametangaza kwamba kwa mwaka 2019 vyombo vya habari vyote ni lazima kupiga nyimbo za dansi.

Kupitia tamasha la uzinduzi wa albam ya bendi ya Twanga Pepeta, ambalo Waziri Mwakyembe alihudhuria ili kusikiliza baadhi ya changamoto ambazo wanazipitia wasanii wa bendi kwa ujumla na kusema kwamba ataanza kutatua matatizo hayo kwa kuhakikisha nyimbo za dansi zinapatiwa vipindi maalumu katika kila chombo cha habari.

"Nawaomba Watanzania wafahamu kwamba muziki wa dansi ni moja kati ya vitu ambayo vilichangia kuleta uhuru katika nchi yetu, nyimbo hizo ndio zilikuwa zinapigwa kwenye kusherehekea na hata katika historia ya nchi nyimbo hizi zipo na hata serikali inatambua uwepo wa nyimbo hizo kwa hiyo nitazipigania kwa kipindi hiki mimi nikiwa nasimamia Sanaa" aliongea  Waziri Mwakyembe.

Naye mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka hakusita kuonyesha furaha yake baada ya kutembelewa na Waziri, huku akimsifia na kusema hajawahi kuona waziri anayependa kazi yake kama  huyu wa sasa ambaye alijitokeza katika kumbi za uswahilini ili kusapoti muziki wa dansi.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini