Lissu Asitishiwa Mshahara Wake Amuwakia Spika Ndugai | ZamotoHabari.

Lissu Asitishiwa Mshahara Wake Amuwakia Spika Ndugai
Tundu Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema,  amemtaka Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai na Katibu wa Bunge hili, Stephen Kagaigai kurejesha mshahara wake na stahiki zake za kibunge.

"Lissu amesema amesitishiwa mshahara na posho za kibunge tangu Januari 2019 bila kuelezwa sababu zozote za hatua hiyo na kusema anakusudia kuchukua hatua za kisheria kufikisha suala hilo, Mahakama Kuu ya Tanzania kudai haki zake.

Mnadhimu huyo Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ametoa malalamiko hayoJumatano Machi 13, 2019 kupitia waraka uliosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ukizungumzia jinsi anavyonyimwa stahiki zake za msingi akiwa mbunge.

"Lissu amesema tangu Septemba 7, 2017 ameshindwa kuhudhuria shughuli za kibunge kutokana na kuwa nje ya nchi baada ya kushambuliwa na risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana kisha kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi.

Katika waraka huo, Lissu amezungumzia sheria na taratibu ambazo mbunge anaweza kukosa sifa ya kuwa mbunge ambazo yeye bado anazo ni pamoja na mtu kuhama chama, kuteuliwa kuwa makamu wa Rais au kuchaguliwa kuwa Rais.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini