Mfahamu Binti aliyefariki, Maiti yake ikaonekana miaka miwili baadaye akiwa bado anatizama runinga | ZamotoHabari.


Anaitwa Joyce Carol Vincent Alikuwa ni Raia wa Uingereza aliyezalliwa tarehe 19 October 1965 na kufariki December mwaka 2003 akiwa na miaka 38


Mwili wa binti huyu ulipatikana katika chumba ambacho alikuwa akiishi miaka miwili mbele baada ya kifo chake, inasemekana kuwa kilichomuuwa binti huyu huenda ikawa ni Athma ambayo ilikuwa inamsumbua kwa muda mrefu, kwa mujibu wa wataalam walioupima mabaki ya mwili wake walibaini kuwa yawezekana ni Athma ilimuuwa kwa kushtukiza au labda ni peptic ulcer ndio iliyomuuwa lakini hawakuwa na uhakika

Mwili wake ulikuwa umeshakaa muda mrefu wa miaka miwili bila kujulikana kwa sababu kodi ya nyumba aliyokuwa anaishi pamoja na gharama za umeme na maji alikuwa akilipiwa na shirika la kanisa

Na kitu kilichoushangaza ulimwengu ni mnamo januari mwaka 2006 mwili wake ulivyokutwa akiwa amekaa kwenye sofa akiangalia tv lakini kumbe ni miaka miwili ilishapita tayari ameshafariki na mwili wake ulikuwa ushaoza na kubakia mifupa tu lakini cha kushangaza alikuwa amekaa pale pale kwenye sofa na tv ilikuwa bado ikiwaka kwa kipindi chote kile


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini