Polisi nchini Italia imemtia mbaroni bwana mmoja mwenye miaka 46 kwa tuhuma za kumtumia mtoto wake mwenye miaka nane kwenye biashara ya dawa za kulevya. Mtoto huyo alifunzwa kusaidia genge la uuzaji dawa za kulevya, ambalo linaaminika kuongozwa na baba yake. Genge hilo kwa mujibu wa mamlaka ni katili katika kutekeleza shughuli zake. Mvulana huyo alifunzwa kutambua tofauti ya dawa mabazo zinauzwa na genge hilo.
Kwa mujibu wa polisi, baba wa mtoto huyo anaitwa Agostino Cambareri, na ni miongoni mwa watu 13 waliokamatwa kutoka kwenye genge hilo. Genge hilo lilikuwa linatumia mawasiliano ya siri kupitia majina na vifaa vya magari na mvulana huyo wa miaka nane alikuwa akijua siri zote hizo kama alivyofunzwa na Bw Cambareri. Washukiwa hao wanadaiwa kuwa walikuwa wakiuza bangi na cocaine katika miji ya kusini magharibi mwa Italia. Pia wanashukiwa kuwa na mahusiano ya karibu na genge kubwa na hatari zaidi la Calabrian ‘Ndrangheta’. Kati ya watu 13 waliokamatwa, nane wapo kizuizini.
Chanzo BBC.
By Ally Juma
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA
0 Comments