Lema amesema Tanzania inapaswa kutoa kauli kali zaidi dhidi ya mauaji yaliyotokea Afrika Kusini | ZamotoHabari.


Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema mataifa mengine na Afrika ikiumizwa ni wote wameumizwa, hivyo Tanzania inapaswa kuwa na kauli kali zaidi.

Kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter aliandika ujumbe hui leo kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Palamagamba Kabudi amefanya vyema kuhakikishia raia wa Afrika Kusini usalama wao.

Lema alisema waziri huyo amesema hakuna mtanzania aliye kufa katika mauaji ya wageni Afrika Kusini.

“Ni heri kwetu lakini mataifa mengine na Afrika ikiumizwa ni sisi wote tumeumizwa, Tanzania inapaswa kuwa na kauli kali zaidi,” aliandika Lema katika ukurasa wake.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipo
BOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini