Kisa cha Ben Pol na Mpenzi Wake ANERLISA Kuogopa Kupata Mtoto | ZamotoHabari.


Mkali wa RnB  Bongo Ben Pol amesema suala la kupata mtoto linapendeza zaidi watu wakiwa kwenye ndoa, pia hatarajii kupata mtoto kwa hivi sasa mpaka atapoingia kwenye ndoa na mpenzi wake Anerlisa Muigai.


Akifunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital,  Ben Pol amesema mpenzi wake huyo hana  ujauzito huwa anaonekana kwenye picha kwa sababu inategemea na pozi la picha.

"Mpenzi wangu sio mjamzito sisi hatuna haraka ya kupata mtoto vitu kama hivyo vinapendeza mkiwa kwenye ndoa, kuzaa na mtu kabla ya ndoa sidhani kama ni sahihi japokuwa watu wengi wanafanya hivyo tufuate taratibu kama wazazi na mungu wanavyotaka" ameeleza Ben Pol 

Aidha  akizungumzia suala kuchelewa kwa ndoa yao Ben Pol amesema  "Hakuna kitu chochote kinachokwamisha ni muda tu ukifika, unajua sisi tunapanga yetu lakini Mungu naye anapanga ya kwake kwa hiyo hata sisi tunacheza na kalenda yake"

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini