Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kichama wa Ilala Jijini Dar es Salaam, Dkt. Milton Makongoro Mahanga amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Machi 23, 2020 katika Hospitali ya taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu tangu juzi.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Ilala, Jerome Olomi amethibitisha kutokea kwa msiba huo na kusema taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitatolewa baadaye.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments