Wanasayansi wa Uturuki Waivalia Njuga CORONA Waanza Kutafuta Mwarobaini wa Kutibu | ZamotoHabari.



Fahrettin Altun, waziri wa habari wa Uturuki amesema wanasayansi na watafiti wa Uturuki wanafanya kazi bila kuchoka katika kuhakikisha wanapata suluhisho la mlipuko ulioikumba dunia wa virusi vipya vya Corona (Covid-19).

 Altun, kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika ujumbe kwa lugha ya kiingereza akisema kazi kubwa imefanyika nchini Uturuki kuzuia kuonekana kwa  kesi za virusi vipya vya Corona.

Altun alisisitiza kwamba hatua madhubuti zitaendelea kuchukuliwa  kuhakikisha mlipuko huo unadhibitiwa.

“Mpaka hivi sasa kuna kesi moja nchini kwetu. Mtu huyo amewekwa karantini na anaendelea na matibabu. Tumetoa taarifa kwa umma na jamii ya kimataifa juu ya suala hili na hatua tulizochukua kwa wakati. Kuhusiana na suala hili tutaendelea kuwa wawazi.

Mwisho Altun alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kufanya kazi pamoja katika kutafuta suluhu ya tatizo hili.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini