Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison, amesema kuwa Simba walikuwa wana uhuru wa kuzungumza naye ili kumpa dili kwa kuwa yeye ni mchezaji mzuri na anajua uwezo wake alionao habahatishi.
Kiungo huyo mwenye mabao matatu alikuwa anawindwa na wapinzani wa Yanga ambapo walitaka kuipata saini yake jambo lililokwama mwishoni baada ya Yanga kumpa dili la miaka miwili.
Morrison amesema kuwa ilikuwa ni rahisi kwake kuingia kwenye akili za Simba kwa kuwa ni mchezaji mzuri na wao wana haki ya kufanya hivyo.
"Ilikuwa ni haki yao kunifuata na kuzungumza nami ili kupata saini yangu kwa kuwa mimi ni mchezaji mzuri na ninaipenda kazi yangu.
"Walinifuata kabla ya mechi yetu dhidi ya Yanga ambapo tulishinda na kupata pointi tatu, nililiacha suala hilo mikononi mwa wakala wangu," amesema.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments