Mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea, amesema kuwa yeye na Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu ni ndugu na ni marafiki wa karibu, kwani huwa wanashirikiana kwenye mambo mbalimbali lakini urafiki huo, haumfanyi afuate kila kitu anachokifanya Komu.
Hayo ameyabainisha leo Aprili 2, 2020, jijini Dar es salaam na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakidhani lazima na yeye atafuata maamuzi ya rafiki yake Komu na kuwataka waache hizo ramli na kwamba hana mpango wa kuhama CHADEMA na ataendelea kuwa Mbunge kupitia chama hicho.
"Komu siyo tu Mbunge mwenzangu bali ni ndugu yangu kabisa, lakini urafiki wangu na Komu haunifanyi nifanye kila kitu anachofanya, mimi bado ni Mbunge wa CHADEMA na nadhani natakiwa kuwatumikia wananchi wangu hadi pale muda utakapomalizika, watu waache ramli tufanye kazi, muda ukifika tutazungumza hayo mambo" amesema Mbunge Kubenea
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments