Mpenzi wa msanii nyota wa Tanzania Diamond Platinumzi Tanasha Donna amesema inawezekana kukaa karantini bila starehe, familia na simu wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona.
Tanasha ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa instagram wakati huu ambao nchi nyingi zinasisitiza raia wake kujitahidi kukaa ndani kama hawalazimiki tutoka nje sababu ya ugonjwa virusi vya Corona.
Mzazi mwenzake huyo na Diamond ambaye ni raia wa Kenya amemposti Rais wa Zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela na kuandika kuwa “In isolation for 27 years, No family, Luxuries, Phone. Just hope and vision, We can do this”.
Mpaka sasa nchini Kenya visa vya Corona vilivyoripotiwa ni 122 na tayari watu wanne wamefariki na nchini Tanzania visa ni 20 na aliyefariki ni mmoja
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments