Mbowe "Ugonjwa wa Corona Bado Haujapewa Uzito Unaotakiwa" | ZamotoHabari.


Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Bunge, Freeman Mbowe, amesema kuwa suala la Corona halijapewa uzito unaostahili huku akishauri kuundwa kwa kikosi kazi cha Taifa kwa ajili ya kuangalia athari za uchumi za ugonjwa huo.

Akichangia leo hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2020/21, Mbowe amesema “Bado suala hili halijapewa uzito unaostahili kama mataifa mengine kwasababu bado kuna uzembe kwa kujua ama kutojua au kudhani liko mbali na halipo nchini, nilitegemea uwepo mpango maalum na kutoa taarifa iwapo kuna athari gani katika uchumi lakini bajeti ziko pale pale.”

Amebainisha kuwa sekta ya utalii imeanguka kwa asilimia 99 na kwamba kuna makampuni yamefungwa huku mapato ya nchi yatapungua kwa asilimia 40 kwa miezi sita ijayo.

“Kumekuwa na kauli tofauti,mikusanyiko ambayo haifai na kwamba kuna mikusanyiko ambao wakuu wa mikoa ndio wamekuwa wakiifanya
Wanakusanya watu, wanahutubia watu kwamba ugonjwa uko mbali hii ni hatari,”amesema.

Ameongeza “Ningetamani tumesikilize Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya kama
nchi ikienda kwa kila kiongozi kutoa taarifa ugonjwa huu utawafikisha mahali pabaya.”

Amesema jambo hilo linahitaji kikosi cha Taifa kwa ajili ya kuangalia athari za uchumi na kijamii na pia kuangalia vipaumbe vya Taifa hivi sasa ni vipi.

APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini