Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania (TALGWU) Suleiman Kikingo amewataka wawakilishi wa vijana wa chama hicho kutekeleza ipasavyo majukumu yao kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu na kuwa wasemaji wazuri wa chama ikiwa ni pamoja na kuyatangaza mafanikio yaliyokwishapatikana ili kujenga Taswira njema kwa wanachama walio ndani hata kwa wale wasio wanachama wa TALGWU.
Kikingo ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili kwa wawakilishi wa vijana wa TALGWU Mikoa ambapo amesema vijana hao hawana budi kuwa mstari wa mbele kusambaza taarifa njema na kuachana na baadhi ya mitandao ambayo imekuwa na dhamira isiyo njema ya kuharibu chama kwa kusababisha migogoro na migongano isiyo na lazima.
“Achaneni na maneno ya mitandaoni yanayoandika habari potofu na mnajua kwanini yanaandika ,maana tayari yanachukuliwa hatua , Katibu mkuu tayari anayashughulikia kwa hivyo niseme muwe wasemaji wazuri na muyafikishe haya tunayoyafanya hata nje ya chama.”Amesema Kikingo.
Amesema kitu cha msingi ni kudumisha umoja na mshikamano ili kujenga taswira njema na hali hiyo itaongeza nguvu katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wanachama.
“ Chama kimefanya mambo mengi makubwa katikakusimamia haki za wafanyakazi kama suala la kikokotoo na haikuwa kazi rahisi lakini kwa kushirikiana kwa karibu sana na TUCTA tulipigana kufa na kupona na viongozi wenzangu mpaka suala lile likaisha vizuri.”Ameongeza
Kwa upande wake Katibu mkuu wa TALGWU Taifa Rashid Mtima amesema wao kama viongozi wakuu wa chama wameona haja ya muda mrefu ambayo kuna mazingira yaliyowakwamisha kutofanya vikao vya pamoja na hivyo vijana waliopata nafasi ya kuwawakilisha vijana wenzao ni lazima watambue kuwa wanao wajibu wao na watambue nini chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa,wajue majukumu yao na wajibu wao kutoka katika maeneo wanayotoka.
“Nyinyi Vijana ndio mfano mzuri kabisa wa kubadilisha fikra na mitizamo ya vijana kutopenda vyama vya wafanyakazi kuliko hao wengine ,kwa hiyo haja ya nyinyi kukutana kuwanoa ,kuwapa misingi ya vyama vya wafanyakazi ,kuwaambia uwepo wa vyama vya wafanyakazi sio bahati.”Amesema
Naye Mwakilishi wa vijana wa TALGWU Taifa Ibrahim Swalehe amesema yapo mambo toka kuanzishwa kwa chama hicho yamefanywa ikiwemo muundo wa uajiri ambapo chama kiliona ni vyema kikaajiri watumishi wa TALGWU wanaotokana na serikali za mitaa ikiwa ni moja ya badiliko kubwa ambalo limekuwa shirikishi kwa jamii wanayoihudumia.
“Hili lilitoa fursa kwa waajiri wa serikali za mitaa ,tuwe waajiriwa wa chama na tuwatete wanachama wenzetu ,leo makatibu wetu wa mikoa wasipofanya vizuri kuna wakati huwa wanasutwakutokana na kutowajibika katika nafsi zao.”Amesisitiza.

Mwenyekiti wa TALGWU Taifa, Suleiman Kikingo akifungua mkutano wa wawakilishi wa vijana Mikoa uliofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TALGWU Taifa, Suleiman Kikingo akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Vijana baada ya kumaliza kufanya mkutano wa pamoja.
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments