Mchekeshaji Ebitoke amefunguka kusema anamchukia Gigy Money kwa sababu anaropoka hovyo na amem-block tangu anaanza kujulikana mwaka 2016, pia amemtaka asijifananishe na Nandy kwani sio levo zake.
Ebitoke amesema hamkubali kabisa Gigy Money kwani aliwahi kumsikia akimuongelea kwenye mahojiano jambo ambalo hakupendezwa nalo.
"Wapo ambao nina tofauti nao ila siwezi nikasema ila kiuhalisia wanawake huwa hatukubaliani, Nikiongelea kuhusu Gigy Money na Nandy kwanza mimi simkubali Gigy halafu huwezi ukamfananisha na Nandy yeye anaropoka kila kitu hawezi kuweka siri, nimewahi kumsikia anaropoka kuhusu mimi na ameni-block tangu naanza kujulikana mwaka 2016, simuogopi na hata moto aliokuwa nao na mimi nauweza" amesema Ebitoke
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa
KUBOFYA HAPA
0 Comments