*Suleman aahidi kuendelea kuratibu matembezi ya Uhuru.
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
WAFANYABIASHARA wameombwa kusaidia sekta ya elimu kwa wanafunzi wa awali katika kuwajengea uwezo wa kujifunza lugha ya kiingereza ili wanapofikia elimu ya juu kuwa na uelewa ikiwa ni Pamoja kuwaweka kiushindani katika wa usaili wakati wanaomba kazi inayohusisha lugha hiyo.
Hayo aliysema Mkurugenzi na Muasisi wa shule ya Awali ya Meadows Academy Mohamed Arif Suleman wakati wa matembezi ya Uhuru yaliyofanyika umbali wa Kilomita 10.3 katika Barabara za Masaki jijini Dar es Salaam.
Katika matembezi hayo wanafunzi wa Sekondari na msingi walikuwa wanajibu maswali yanayoaulizwa kwa njia ya mtandao kwa kutumai simu janja.
Suleman amesema matembezi hayo ni ya mara ya sita tangu kuanzishwa kwa kushirikisha shule za mbili za Sekondari na Msingi ambazo Sekondari ni Oasterbay pamoja na Bongoyo.
Amesema kwa kutambua watu wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto walishirikisha vituo viwili ambavyo ni Mazila na Ophanage Of Good Hope.
Aidha amesema katika kutambua kwa kundi hilo huchukua watoto wawili katika shule hiyo pamoja na kusaidia baadhi ya shule vitabu na mahitaji mengine kwa kuamini wanawajibu wa kushirikiana na jamii.
Naye mwanafunzi wa shule ya Sekondari Oasterbay kidato cha Tatu Daud Joseph amesema katika matembezi hayo wamejifunza vitu vingi ikiwemo na kujenga mwili kiafya.
Amesema kuwa wanashukuru matembezi hayo yanayoratibiwa kwa kuwa na vitu vya kujifunza masuala ya teknolojia.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Christina Mpili amesema kuwa waandaji waendelee kuwashirikisha kwani wanakutana na wanafunzi wengi kutoka shule mbalimbali.
*Suleman aahidi kuendelea kuratibu matembezi ya Uhuru.
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
Wafanyabiashara wameombwa kusaidia sekta ya elimu wanafunzi wa awali katika kuwajengea uwezo wa kujifunza lugha ya kiingereza ili wanapofikia elimu ya juu kuwa na uelewa ikiwa ni Pamoja kuwaweka kiushindani katika wa usaili wakati wanaomba kazi inayohusisha lugha hiyo.
Hayo aliysema Mkurugenzi na Muasisi wa shule ya Awali ya Meadows Academy Mohamed Arif Suleman wakati wa matembezi ya Uhuru yaliyofanyika umbali wa Kilomita 10.3 katika Barabara za Masaki jijini Dar es Salaam.
Katika matembezi hayo wanafunzi wa Sekondari na msingi walikuwa wanajibu maswali yanayoaulizwa kwa njia ya mtandao kwa kutumai simu janja.
Suleman amesema matembezi hayo ni ya mara ya sita tangu kuanzishwa kwa kushirikisha shule za mbili za Sekondari na Msingi ambazo Sekondari ni Oasterbay pamoja na Bongoyo.
Amesema kwa kutambua watu wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto walishirikisha vituo viwili ambavyo ni Mazila na Ophanage Of Good Hope.
Aidha amesema katika kutambua kwa kundi hilo huchukua watoto wawili katika shule hiyo pamoja na kusaidia baadhi ya shule vitabu na mahitaji mengine kwa kuamini wanawajibu wa kushirikiana na jamii.
Nae mwanafunzi wa shule ya Sekondari Oasterbay kidato cha Tatu Daud Joseph amesema katika matembezi hayo wamejifunza vitu vingi ikiwemo na kujenga mwili kiafya.
Amesema kuwa wanashukuru matembezi hayo yanayoratibiwa kwa kuwa na vitu vya kujifunza masuala ya teknolojia.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Christina Mpili amesema kuwa waandaji waendelee kuwashirikisha kwani wanakutana na wanafunzi wengi kutoka shule mbalimbali
APP YETU MPYA: Sasa unaweza kusoma kwa urahisi kupitia APP yetu. Download hapa kwa KUBOFYA HAPA
0 Comments